Friday, 17 June 2016
SIRA YA MTUME MUHAMMAD PANGO LA HIRAA
Mtume S.A.W alipokaribia kufikia umri wa miaka 40, alianza kupenda kujitenga na watu na kufanya ibada.
Alikua akichukua chakula chake na maji na kwwenda katika Pango la Hiraa lililopo katika Mlima Nur (Jabal Nur)
kiasi cha umbali wa maili mbili kutoka Makka.
Aliendelea kukaa katika pango hilo kwa muda wa mwezi mmoja akiwalisha maskini waliokuwa wakimuendea huko. Alitumia wakati wake mwingi kufanya ibada na kutafakari masuala yaliomzunguka katika mazingira ya hususan akishughulishwa sana na ysle yanayofanywa na na watu yanayohusiana na ushirikina na la ubaya zaidi, hakuwa na njia ya wazi mbele yake ya kuifuata ili kuondosha yale mabaya anayoyaona kwa watu wale.
Kuamua kwa Mtume S.A.W kujitenga na watu na kutafakari yale yanayofanywa na watu ilikua ni njia miongoni mwa njia za Mwenyezi Mungu za kumuandaa kwa jmabo kubwa lililokua lilkimsubiri mbele yake.
Alipotimiza miaka 40 katika maisha yake zikaanza kumtokea alama za utume. Alama hizo zilikua ni ndoto za kweli. Ikawa haoti kitu usiku isipokua asubuhi kitatokea kweli vilievile alivyokiota usiku. Hali hii ikaendelea kwa muda wa miezi 6.
Ulipoingia mwezi wa Ramadhani wa mwaka wa tatu tokea aaanze kujitengena watu: Mwenyezi Mungu akampa Utume, kwa kuteremkiwa na Malaika Jibril amabae alismoea aya za mwanzo za Qur'an.
Siku aliyoteremkiwa Bwana Mtume S.A.W na Jibril na kupewa Utume ilikua siku ya Jumatatu ya tarehe 21 mwezi wa Ramadhani sawa na tarehe 10 Agosti Mwaka 610(10/8/610) Miladia. Wakati huu umri wake ulikua umetimia miaka 40 ya muandamo wa mwezi (Qamariyya) na miezi sita na siku 12 sawa na miaka 39 ya jua (Shamsiyya) na miezi mitatu na siku 12.
Jibril Anamtokea Bwana Mtume S.A.W
Wakati alipokua katika lile pango la Hiraa akatokea Malaika Jibril na akamwambia SOMA!, Mtume S.A.W akajibu "Mimi si mwenye kusoma". Malaika Jibril akamchukua Mtume na kumbana katika kuta za Pango hilo! na kisha akamuachia na kisha akamwambia tena SOMA!, Mtume S.A.W hakua na jibu lengine zaidi la lile la mwanzo akamjibu tena, "Mimi si mwenye Kusoma". Malaika Jibril akamchukua tena kwa mara ya pili Mtume na kumbana katika kuta za Pango hilo! na kisha akamuachia na kisha akamwambia tena SOMA!, Mtume S.A.W hakua na jibu lengine zaidi la lile la mwanzo akamjibu tena, "Mimi si mwenye Kusoma". Malaika Jibril akamchukua tena kwa mara ya tatu Mtume na kumbana katika kuta za Pango hilo! na kisha akamuachia na kisha akamwambia tena SOMA KWA JINA LA MOLA WAKO ALIEUMBA, AMEUMBA MWANADAMU KUTOKANA NA PANDE LA DAMU, SOMA NA MOLA WAKO NI MKARIMU MNO.
Mtume alistuka mno, na akarudi kwa bi Khadija na huku moyo ukimpiga kwa hofu, akaingia ndani huku akisema "Nifunikeni, nifunikeni", wakmafunika mpaka ile hofu ilipomuondoka.
Alipomuhadithia mkewe juu ya lile tukio na kusema "niliingiwa na woga juu ya nafsi yangu", basi bi Kadija akamwambia , "Katu naapa kwa Mwenyezi Mungu ya kuwa yeye hatokuaibisha hata mara moja na hakika wewe utaunga udugu, utabeba mazito, utachuma visivyokuwepo, utakirimu wageni na utasaidia kwenye haki"
Hapo Mtume S.A.W akatoka mpaka kwa Bwana Waraqat bin Nawfal. Huyu alikua ami yake bi Kadija na aliingia katika dini ya kianswara katika zama zile za ujahiliyapale Makka. Yeye alikua anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiebrania ambayo ni lugha ya Nabii Issa (A.S). Pia bwana Waraqat ndie aliekua akiandika INJILI hiyo kwa lugha ya Kiebrania, na aliweza kuandika kwa kiasi alichojaaliwa. Wakati huo alikua tayari ni mtu mzima amezeeka na macho yake yalikua tayari yameingia upofu.
Walipofika kwa bwana Waraqat, bi Khadija akamuambia, "ewe mtoto wa am hebui msikilize mtoto wa ndugu yako".
Akasema bwana Waraqat, kumwambia Mtume S.A.W "Ewe mtoto wa ndugu yangu umeona nini?" Hapo Mtume S.A.W akamueleza yale yoote alioyaona. Waraqat akasema "Huyo ni malaika aliempeleka Mwenyezi Mungu kwa Mussa, ya laiti ningekua nguzo, ya laiti ningekua wakati huo pale watu watakapokutoa katika mji...." Mtume akauliza kwa kumkatisha bwana Waraqat "hivi watanitoa hawa?" Bwana Waraqat akajibu, "hajawahi kupewa mtu yoyoote kwa mfano wa haya uliopewa weweisipokua alifanyiwa uadui, na kama siku zako za utume zikinikuta nitakunusuru". Lakini kwamipango ya Mwenyezi Mungu bwana Waraqat hakuwahi kuishi muda mrefu baada ya hapo, akafariki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment