Tuesday, 20 December 2016

KUSENGENYA

                                                                                                                    اعوذ بالله من الشيطان الرجيم
                                                                                                                        بسم الله الرحمن الرحيم

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.

                                             الغيبة
سئل النبي صلّى الله عليه وسلم ما كفارة الاغتياب؟ فقال: تستغفر الله  لمن اغتبته.

                                                                                                     KUSENGENYA

Kaulizwa bwana  Mtume Swalla-llahu alayhi wasallam, Nini kafara ya kumsemamtu? Akasema: unamuombea maghfira yule unayemsema.

وسأل النبي اصحابه:
اتدرون مالغيبه؟ قالوا: الله ورسوله اعلم. قال ذكرك اخاك بما يكره. قال: افرايت ان كان في اخي ما اقول؟ قال: ان كان فيه ما تقول فقد اغتبته وانلم يكن فيه فقد بهته.

Na Mtume Swalla-llahu alayhi wasallam akawauliza maswahaba zake:
Mnajua ni vipi kumsema mtu? Wakasema: Mwenyezimungu na mtume wake ndio wanaojua. Akasema Mtume Swalla-llahu alayhi wasallam kumsema ndugu yako kwa jambo analolichukia. Akasema mmoja wao: Ikiwa ninalolisema analo ndugu yangu? Akasema Mtume Swalla-llahu alayhi wasallam:imiwa analo unalolisema basi umemsema kwa vibaya, na akiwa hana basi umemsingiziya.

مقال النبي صلى الله عليه وسلم :
الغيبة تفطر الصا ئم وتنقذ الوضوء.

Kusengenya watu kunamvunja saumu mwenye kufunga, na kunatoa udhu...

الكمال لله
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.

Thursday, 30 June 2016

SUTRA



Neno 'Sutra' maana yake ni hifadhi, kinga, himaya, sitara, ulinzi nakadhalika Na maana yake ni kuweka kitu mbele yako unapokuwa unasali ili kitu hicho kiwe kama ni sitara baina yako na baina ya anayetaka kupita mbele yako.



Hukmu yake

Ni vizuri kwa anayesali kujiwekea 'Sutra' (sitara) mbele yake kwa ajili ya kuzuwia mtu asipite mbele yake na ili asiwe akianglia huku na kule wakati wa kusali.

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) amesema:

"Mmoja wenu anaposali ajiwekee Sutra na awe karibu nayo."

Abu Daud na Ibni Majah.

Imepokelewa pia kuwa Masahaba (Radhiyallahu 'anhum) walikuwa wakijiwekea mikuki mbele yao wanaposali wakiwa safarini, na waliofuatailia baada ya Masahaba pia walikuwa wakifanya hivyo.

Maulamaa wanasema kuwa ni vizuri kujiwekea Sutra ikiwa unahofia mtu asipite mbele yako, ama ukiwa huhofii basi si lazima, na hii inatokana na hadithi iliyosimuliwa na Imam Ahmad na Abu Daud na Al Baihaqiy kuwa Ibni Abbas (Radhiyallahu 'anhu) alisali mahali penye uwazi na hakuweka mbele yake kitu chochote.



Vipi inapatikana Sutra?

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) amesema:

"Anaposali mmoja wenu basi ajiwekee Sutra mbele yake hata kama ni mkuki."

Ahmad na Al Hakim

Na katika hadithi nyingine:

"Ikiwa hajapata mkuki basi hata fimbo."

Na akasema:

"Anaposali mmoja wenu ajiwekee kitu mbele yake, na asipopata kitu basi hata fimbo, na kama hana fimbo basi achore msitari na hatodhurika na yeyote atakayepita mbele yake."

Ahmad na Abu Daud na wengine

Imepokelewa pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) amewahi kusali akiielekea nguzo (kama ni Sutra), na amesali kukielekea kitanda huku Bibi Aisha (Radhiyallahu 'anhaa) akiwa amelala juu yake, na amesali kuulekea mti nakadhalika.



Sutra ya Imam ni Sutra ya maamuma

Sutra ya Imamu ni Sutra ya maamuma wote walio nyuma yake.

Kutoka kwa Amru bin Shuaib, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake amesema:

"Tulikuwa safarini pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) katika njia iliyonyanyuka karibu na Makkah, na ulipowadia wakati wa Sala akatusalisha akiwa ameuelekea ukuta na kuufanya kuwa kibla na sisi tukiwa nyuma yake. Kondoo akataka kupita mbele yake, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) akawa anamzuwia asipite mpaka akamlazimisha apite nyuma yake."

Imam Ahmad na Abu Daud.

Na kutoka kwa Ibni Abbas (Radhiyallahu 'anhu) amesema:

"Nilikuwa nimepanda punda na wakati huo nilikuwa nishabaleghe na Mtume (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) alikuwa akisalisha watu Mina, nikapita mbele ya baadhi ya safu za watu wanaosali nyuma yake, nikampumzisha punda na kuingia ndani ya safu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) hakunikataza."

Imepokelewa na maimam wote

Na hizi ni dalili kuwa haijuzu kupita mbele ya imamu, lakini inajuzu kupita mbele ya safu za maamuma kwa sababu Sutra ya imamu ni Sutra ya maamuma.



Haramu kupita mbele ya anayesali

Anasema Abu Juhaym kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) amesema:

"Lau kama angejuwa malipo yake (dhambi zake) mwenye kupita mbele ya anayesali, basi angehiari kungoja arubaini kuliko kupita mbele yake."

Hakutaja kama hizo 40 ni siku au miezi au miaka.

Imepokelewa na maimamu wote.



Wakiisherehesha hadithi hii, maulamaa waanasema:

"Hii kama anasali akiwa ameweka mbele yake Sutra. Ikiwa hajaweka Sutra basi si haramu kupita mbele yake. Na ikiwa amejiwekea Sutra, basi anayo haki ya kumsukuma na kumzuwia yeyote asipite mbele yake awe ni mwanadamu au mnyama."

Imepokelewa kuwa siku moja Abu Said al Khodari (Radhiyallahu 'anhu) alikuwa akisali na mtu mmoja alijaribu kupita mbele yake, na Abu Said (Radhiyallahu 'anhu) akamzuwia na alipojaribu kupita kwa nguvu akamsukuma.

Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo akasema:

"Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallahu Llahu alayhi wa Sallam) akisema:

"Mmoja wenu akisali na mbele yake amejiwekea Sutra kujisitiri na watu, basi mtu yeyote akitaka kupita baina yake na baina ya Sutra hiyo amzuwie na akikataa apigane naye kwani huyo ni shetani."

Bukhari na Muslim

SWALI?

Aslam aleykum kuna swali linanitaza ninaomba ufafanuzi.

Mimi ninaishi marekani ya kaskazini. Ninapokwenda msikitini baada kumaliza kutia udhu kutokana na baridi kali ya marekani inanibidi tujifute maji ya udhu.

Je kidini inakubalika kuufuta udhu naomba jibu



Majibu;

Anasema Imam Annawawiy kuwa ipo khitilafu baina ya maulamaa katika Masaala ya kupangusa maji baada ya kutia udhu. Wapo wanaosema kuwa ni Makruh na wapo wanaosema kuwa Inajuzu na hapana ubaya wowote., lakini hapana anayesema kuwa kupangusa kunavunja udhu juu ya kuwa maulamaa wengi wanaona kuwa hapana ubaya wowote katika kupangusa.

Wanaosema kuwa ni Makruh, dalili yao ni ile hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) siku ile alipoletewa kitambaa na Bibi Maymuna (RA) kwa ajili ya kujipangusia nacho maji baada ya kutawadha, na Mtume (SAW) akakirudisha kitambaa kile bila kujipangusia nacho

Wanasema kuwa kwa vile Mtume (SAW) hakujipangusa, hii ni dalili kuwa kuacha kujipangusa ni bora kuliko kujipangusa, wakati huo huo ingekuwa haijuzu kujipangusa basi Mtume (SAW) lazima angewajulisha juu ya hilo.

Na hii ndiyo hoja waliyonayo wengi miongoni mwa maulamaa kuwa hapana ubaya kujipangusa maji baada ya kutawadha, hasa panapo udhuru kama vile baridi

ADABU ZA MSALANI

Muislamu anatakiwa afuate mafunzo ya dini yake katika harakati zake zote,hata anapotaka kwenda haja basi atambue adabu na mafunzo ya Uiislamu kisha afuate.

Nijambo la msingi kufahamu kuwa sehemu za kufanya haja (choo) ni moja kati ya makaazi makuu ya Sheitani, hivyo muislamu anatakiwa achukue kila tahadhari na kufuata miongozo ya Uislamu ili asidhurike na viumbe hivi vibaya. Kuna adabu nyingi za kwenda haja, ambazo Uislamu umetufunza katika hali tofauti,miongoni mwa hizo nikama zifuatazo :



1).Kuhakikisha kuwa upo mbali na watu ikiwa unataka kufanya haja sehemu ya wazi, pia jiepushe na sehemu zifuatazo: sehemu yenye kivuli wanachotumia watu kwa mapumziko.

Amesema mtume (s.a.w);

"Jiepusheni na laana tatu (nazo ni) kufanya haja katika vianzio vya maji, njiani na kwenye kivuli.".

Pia chini ya mti wenye matunda, kwenye maji kidogo yaliyotuama.

Amesema mtume(s.a.w);

"Asifanye mmoja wenu haja ndogo katika maji yaliyotwama kisha akakoga ndani yake."



2) Wakati wa kuingia sehemu ya haja.Unapotaka kuingia tanguliza mguu wa kushoto huku ukisema maneno haya;

"Allahumma inniy audhu bika minal khubuthi wal khabaith."

Na maana yake ni; "Mola wangu, najilinda kwako na shari ya majini wa kiume na majini wa kike."



3) Baada ya kuingia chooni. Kabla ya kuanza kufanya haja ni vizuri kuhakikisha kuwa maji au mawe ya kujitoharisha yapo kwani alikuwa Mtume (SAW) akiandaa maji katika chombo kabla yakufanya haja. pia inakatazwa mtu kuzungumza au kuimba au hata kufanya zogo hadi kusikia walio nje.



4) Wakati wa kufanya haja. Utaegemea mguu wako wa kushoto wakati wa kufanya haja hali ya kuwa umechuchumaa kwani inasaidia kutoka uchafu kwa wepesi, na kwa hali yoyote ile jiepushe na kufanya haja ukiwa umesimama. Usiangalie utupu, wala kile kinachotoka, na asikichezee, pia usiangalie mbinguni au kugeuka kulia na kushoto, usielekee kibla wala usikipe mgongo ikiwa unakwenda haja sehemu ya wazi.

Amesema Mtume ( SA W);

"Anapotaka kufanya haja mmoja wenu asielekee kibla wala asikipe mgongo."

Na wala usilielekee jua pale linapozama au linapochomoza. Jihadhari na cheche za kile kinachotoka, kwani Mtume (SA W) amesema;

"Ataadhibikiwa ndani ya kaburi yule asiyejiepusha na cheche (za haja ndogo na kubwa)".



5) Baada ya kumaliza kufanya haja zako unatakiwa uhakikishe kuwa hakuna kitu kinachobaki, hivyo unatakiwa ufanye kila njia ili kuhakikisha kuwa uchafu umekwisha, kisha anza kujisafisha kwa kutumia mawe masafi kisha malizia kwa maji, na inatosha kutumia maji matupu bila ya mawe, na pindi ukikosa maji basi mawe yanatosha lakini kwa kutimiza shuruti zake ambazo zimetajwa kwenye vitabu vya fiqhi, pia jiepushe kujisafisha kwa kutumia mifupa au chakula kwani ni miongoni mwa kukufuru neema ya Mola wako, jisafishe kwa kutumia mkono wako wa kushoto na kuanzia sehemu inayotoka haja ndogo.



6) Baada ya kujitoharisha.Usikae kwa muda mrefu pale ulipofanyia haja kwani inasababisha ugonjwa wa ini kama ilivyopokewa kutoka kwa Lukman. Baada ya hapo vaa nguo zako kisha utawadhe kama udhu wa sala 7) Wakati wa kutoka. Unapotaka kutoka tanguliza mguu wako wa kulia huku unasema;

"Ghufraanaka - Ewe Mola nakuomba unisamehe, namshukuru Allah aliyeniondoshea yanayoniudhi na kunibakishia yanayoninufaisha"

SIJDA YA KUSAHAU


Imethibiti kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amewahi kusahau ndani ya Sala, na imethibiti pia kuwa aliwahi kusema:

"Hakika mimi ni mwanadamu, ninasahau kama mnavyosahau, kwa hivyo ninaposahau nikumbusheni."



Hukmu

Sajda ya kusahau (Sujuud al Sahau) inasujudiwa mara mbili kabla ya kutoa salamu au baada yake, na imesihi kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alifanya namna zote mbili.

Katika hadithi sahihi, amesema Abu Said al Khudary (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Mmoja wetu akitia shaka ndani ya sala yake akawa hana uhakika amesali rakaa tatu au nne, basi aache kutia shaka na ahesabu zile alizo na uhakika nazo, kisha asujudu sajda mbili kabla ya kutoa salamu."

Sharhi:

Maana ya kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliposema: "Aache kutia shaka na ahesabu zile alizo na uhakika nazo" ni kuwa; Mtu anapokuwa ndani ya sala akatia shaka iwapo yupo katika rakaa ya tatu au ya nne, huwa na hakika kuwa wakati ule kesha Sali rakaa tatu, isipokuwa ile ya nne ndiyo anayoitilia shaka. Kwa ajili hiyo anatakiwa ahesabu zile tatu tu alizo na uhakika nazo – na asali rakaa moja tu kwa ajili ya kukamilisha rakaa nne, kisha asujudu sajda ya kusahau.



Sababu za kusujudu

Mtu anaposahau akatoa salamu kabla ya kukamilisha sala;

Na hii inatokana na hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibni Siriyn kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

"Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) sala mojawapo za mchana, (adhuhuri au alasiri) akasali rakaa mbili kisha akatoa salamu kisha akainuka na kukaa akiwa ameegemea nguzo akionesha dalili ya kughadhibika, na Abubakar na Omar (Radhiya Llahu anhu) walikuwepo, na alikuwepo pia mtu mmoja anayejulikana kwa jina la 'Dhul Yadayni' aliyeuliza:

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, umesahau au umefupisha?"

Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema:

"Sijasahau wala sijafupisha.", kisha Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akauliza:

"Ni kweli maneno anayosema Dhul Yadayni?"

Wakamwambia:

"Ndiyo."

Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akainuka, akatangulia mbele (mahali aliposimama alipokuwa akisalisha), kisha akakamilisha rakaa mbili alizozisahau, kisha akatoa salamu, kisha akasema: "Allahu akbar", kisha akasujudu sajda kama ya kawaida au ndefu zaidi kidogo, kisha akakaa, kisha akasema tena: "Allahu akbar," kisha akasujudu tena kama alivyosujudu mwanzo kisha akakaa.

Bukhari na Muslim



Hadithi nyingine

Kutoka kwa Ataa amesema: "Mwana wa Al Zubair (Radhiya Llahu anhu) alisalisha sala ya magharibi kisha akatoa salamu baada ya kusali rakaa mbili, na aliponyanyuka kutaka kulibusu jiwe (la Al Kaaba) watu wakasema: "Subhana Llah!", akarudi na kuwauliza: "Mna nini?" Anasema Ataa: "Akakamilsha rakaa aliyoiacha kisha akasujudu sajda mbili ."

Al Tabarani



Anapoongeza

Imepokelewa pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kusahau akaongeza rakaa moja na watu wakasema: "Subhana Llah", kisha wakamwambia: "Umezidisha rakaa moja, umesalisha tano." Akasujudu sajda mbili baada ya kutoa salamu.



Anaposahau Kusoma Tahiyatu

Imepokelewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kusahau kusoma tahiyatu ya mwanzo na baada ya kumaliza sala akasujudu sajda mbili kisha akatoa salam.



Maamuma anasujudu anaposujudu imamu sajda ya kusahau, lakini anaposahau yeye maamuma hatakiwi kusujudu sajda ya kusahau.



Ndani ya Sajda ya kusahau unasoma dua zile zile unazosoma katika sajda ya kawaida.

Unaweza kusujudu Sajda ya kusahau wakati wowote utakapokumbuka hata kama usharudi nyumbani kutoka msikitini.

Sunday, 26 June 2016

ADABU:MAKRUHU YA KUACHA KUENDELEA KUSOMA QUR'AN KWA AJILI YA MAMBO MENGINE

Yampasa kila msomaji wa qur'an kutoacha kuendelea kusoma qur'an ila kwa jambo la umuhimu si vizuri mtu kukatisha kuacha kusoma qur'an kwa ajili ya mambo yake ya kidunia,kwa masikitiko makubwa wengi wetu waislamu utamuona mtu yupo msikitini kisha huanza kuangalia huku na huku kwa ajili ya kuangalia nani anaingia msikitini kwani tabia kama hiyo hutokana na Sheitwan ambaye hamtakii mema muislam.Imesimuliwa na mmoja kati ya matabii,Naafai amesimulia kwamba Ibn Umar alikuwa aongea neno lingine lolote mpaka amalizapo kusoma Quraan" pia Naafai anaendelea kusema kwamba alikuwa na Ibn umar siku moja alisoma surat Baqara kisha akasimama na akamuuliza unajua hii imeshuka kwa mnasaba gani akamwambia sifahamu,kisha akamuelekeza hii ni kwa sababu fulani na fulani hiyo ni namna Ibn umar alivyo ishi alikua akati usomaji wake wa quraan isipokuwa kwa ajili ya kutoa elimu ambayo ni moja kati ya Ibada.

Friday, 17 June 2016

Khutba ya ijumaa

SIRA YA MTUME MUHAMMAD PANGO LA HIRAA


Mtume S.A.W alipokaribia kufikia umri wa miaka 40, alianza kupenda kujitenga na watu na kufanya ibada.
Alikua akichukua chakula chake na maji na kwwenda katika Pango la Hiraa lililopo katika Mlima Nur (Jabal Nur)
kiasi cha umbali wa maili mbili kutoka Makka.

Aliendelea kukaa katika pango hilo kwa muda wa mwezi mmoja akiwalisha maskini waliokuwa wakimuendea huko. Alitumia wakati wake mwingi kufanya ibada na kutafakari masuala yaliomzunguka katika mazingira ya hususan akishughulishwa sana na ysle yanayofanywa na na watu yanayohusiana na ushirikina na la ubaya zaidi, hakuwa na njia ya wazi mbele yake ya kuifuata ili kuondosha yale mabaya anayoyaona kwa watu wale.

Kuamua kwa Mtume S.A.W kujitenga na watu na kutafakari yale yanayofanywa na watu ilikua ni njia miongoni mwa njia za Mwenyezi Mungu za kumuandaa kwa jmabo kubwa lililokua lilkimsubiri mbele yake.

Alipotimiza miaka 40 katika maisha yake zikaanza kumtokea alama za utume. Alama hizo zilikua ni ndoto za kweli. Ikawa haoti kitu usiku isipokua asubuhi kitatokea kweli vilievile alivyokiota usiku. Hali hii ikaendelea kwa muda wa miezi 6.

Ulipoingia mwezi wa Ramadhani wa mwaka wa tatu tokea aaanze kujitengena watu: Mwenyezi Mungu akampa Utume, kwa kuteremkiwa na Malaika Jibril amabae alismoea aya za mwanzo za Qur'an.

Siku aliyoteremkiwa Bwana Mtume S.A.W na Jibril na kupewa Utume ilikua siku ya Jumatatu ya tarehe 21 mwezi wa Ramadhani sawa na tarehe 10 Agosti Mwaka 610(10/8/610) Miladia. Wakati huu umri wake ulikua umetimia miaka 40 ya muandamo wa mwezi (Qamariyya) na miezi sita na siku 12 sawa na miaka 39 ya jua (Shamsiyya) na miezi mitatu na siku 12.

Jibril Anamtokea Bwana Mtume S.A.W
Wakati alipokua katika lile pango la Hiraa akatokea Malaika Jibril na akamwambia SOMA!, Mtume S.A.W akajibu "Mimi si mwenye kusoma". Malaika Jibril akamchukua Mtume na kumbana katika kuta za Pango hilo! na kisha akamuachia na kisha akamwambia tena SOMA!, Mtume S.A.W hakua na jibu lengine zaidi la lile la mwanzo akamjibu tena, "Mimi si mwenye Kusoma". Malaika Jibril akamchukua tena kwa mara ya pili Mtume na kumbana katika kuta za Pango hilo! na kisha akamuachia na kisha akamwambia tena SOMA!, Mtume S.A.W hakua na jibu lengine zaidi la lile la mwanzo akamjibu tena, "Mimi si mwenye Kusoma". Malaika Jibril akamchukua tena kwa mara ya tatu Mtume na kumbana katika kuta za Pango hilo! na kisha akamuachia na kisha akamwambia tena SOMA KWA JINA LA MOLA WAKO ALIEUMBA, AMEUMBA MWANADAMU KUTOKANA NA PANDE LA DAMU, SOMA NA MOLA WAKO NI MKARIMU MNO.

Mtume alistuka mno, na akarudi kwa bi Khadija na huku moyo ukimpiga kwa hofu, akaingia ndani huku akisema "Nifunikeni, nifunikeni", wakmafunika mpaka ile hofu ilipomuondoka.

Alipomuhadithia mkewe juu ya lile tukio na kusema "niliingiwa na woga juu ya nafsi yangu", basi bi Kadija akamwambia , "Katu naapa kwa Mwenyezi Mungu ya kuwa yeye hatokuaibisha hata mara moja na hakika wewe utaunga udugu, utabeba mazito, utachuma visivyokuwepo, utakirimu wageni na utasaidia kwenye haki"

Hapo Mtume S.A.W akatoka mpaka kwa Bwana Waraqat bin Nawfal. Huyu alikua ami yake bi Kadija na aliingia katika dini ya kianswara katika zama zile za ujahiliyapale Makka. Yeye alikua anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiebrania ambayo ni lugha ya Nabii Issa (A.S). Pia bwana Waraqat ndie aliekua akiandika INJILI hiyo kwa lugha ya Kiebrania, na aliweza kuandika kwa kiasi alichojaaliwa. Wakati huo alikua tayari ni mtu mzima amezeeka na macho yake yalikua tayari yameingia upofu.

Walipofika kwa bwana Waraqat, bi Khadija akamuambia, "ewe mtoto wa am hebui msikilize mtoto wa ndugu yako".

Akasema bwana Waraqat, kumwambia Mtume S.A.W "Ewe mtoto wa ndugu yangu umeona nini?" Hapo Mtume S.A.W akamueleza yale yoote alioyaona. Waraqat akasema "Huyo ni malaika aliempeleka Mwenyezi Mungu kwa Mussa, ya laiti ningekua nguzo, ya laiti ningekua wakati huo pale watu watakapokutoa katika mji...." Mtume akauliza kwa kumkatisha bwana Waraqat "hivi watanitoa hawa?" Bwana Waraqat akajibu, "hajawahi kupewa mtu yoyoote kwa mfano wa haya uliopewa weweisipokua alifanyiwa uadui, na kama siku zako za utume zikinikuta nitakunusuru". Lakini kwamipango ya Mwenyezi Mungu bwana Waraqat hakuwahi kuishi muda mrefu baada ya hapo, akafariki.

Thursday, 16 June 2016

WANAFUNZI WALAZIMISHWA KUSALIMIANA NA WALIMU WAO KWA MIKONO BAINA YA JINSIA MBILI SWITZZERLAND


Wanafunzi wakiislamu wakiume wameagizwa kusalimia walimu wao kwa kushikana mikono au wazazi walipe faini ya (£3,500). hii ilitokana baada ya mwanafunzi mmoja kukataa kusalimiana na mwalimu wake na kusema ni kinyume na dini ya kiislam,serikali ya nchi hiyo wamelijadili suala hilo na kufikia mwafaka kuanzisha sheria hiyo kwani kusalimia kati ya mwalimu na wanafunzi ni moja kati ya Adabu,kwani watoto hao toka wakiwa watoto hulelewa katika maadili ya utiifu kwa wakubwa wao na kuwaambia wanafunzi hao kukataa kusalimiana kwa mikono kwa mgongo wa dini halivumiliki.